Friday, January 30, 2009

NAKAAYA KALA SHAVU SONY

Tanzania songbird NAKAAYA SUMARI signed to SONY MUSIC ENTERTAINMENT making history by being the first East African artist ever to be signed to the second largest record company in the world.Baadhi ya wanamuziki ambao wako under this label ni Beyonce Knowles,Alicia Keys,Chris Brown,Sean Kingstone na wengineo wengi tu wenye majina makubwa.Big up Nakaaya Sumari.
Kwa habari zaidi nenda linki hii hapa;

NICE TRANSITION


Thursday, January 22, 2009

WAWILI WAHUKUMIWA KIFO KWA SCANDAL YA MAZIWA YENYE SUMU(MELAMINE) CHINA

Mwanamke aliyefiwa na mtoto wake baada ya kunywa maziwa yenye sumu akilia kwa uchungu na kuonyesha kipeperushi chake kilichoandikwa nirudishieni mtoto wangu!!
2 death sentences given in China milk scandal
SHIJIAZHUANG, China – A Chinese court condemned two men to death Thursday and handed a life term to a former dairy boss in the first sentences for those involved in the country's contaminated milk scandal.
The Intermediate People's Court in Shijiazhuang gave the life sentence to Tian Wenhua, 66, the former general manager and chairwoman of Sanlu Group Co., the dairy at the center of the crisis. She was the highest-ranking official charged in the food safety scandal, widely seen as a national disgrace that highlighted corporate and official shortcomings and corruption.
At her trial at the end of December Tian pleaded guilty to charges of producing and selling fake or substandard products after infant formula tainted with the chemical melamine was blamed in the deaths of at least six babies and the illnesses of nearly 300,000 others.
The court also sentenced Zhang Yujun, 40, to death for running a workshop that was allegedly China's largest source of melamine, said spokesman Wang Wei. A second man, Geng Jinping, was also given the death penalty for producing and selling toxic food.
Zheng Shuzhen, from Henan province, said her 1-year-old granddaughter died in June after drinking Sanlu milk.
"I've run out of tears. ... That's why I came today. Even if (Tian) dies a hundred times over, it won't lessen our hate," Zheng said.
A total of 21 defendants were being sentenced Thursday in connection with the case.
Two men, including 24-year-old Zhang Yanzhang, were sentenced to life imprisonment for endangering public safety. Zhang Yanzhang was accused of working with Zhang Yujun.
Three other former Sanlu executives were given between five years and 15 years in prison.
The sentences were read out by Wang outside the court, where families of babies sickened in the scandal had anxiously gathered.
In a reflection of the trial's sensitivity, dozens of policers officers guarded the courthouse and cordoned off the surrounding area with plastic barriers. Officers told the victims' families to keep about 100 yards (meters) away.
Sanlu, along with the other 21 dairy companies involved in the scandal, have proposed a 1.1 billion yuan ($160 million) compensation plan. More than 200 families have filed suit demanding higher compensation and long-term treatment for their babies.
Zhao Lianhai, who has set up a Web site to help organize parents whose children were sickened, said about a dozen parents from across the country had hoped to attend the sentencing but only seven showed up.
Authorities detained at least two sets of parents of melamine victims as they attempted to travel to the courthouse, said Li Fangping, a Beijing lawyer who has worked with the parents since news of the poisonings emerged.
Dong Shiliang, from southern Yunnan province, was stopped from boarding a plane in Kunming on Wednesday while Liu Donglin was being held at a Beijing police station, he said.
During her Dec. 31 trial, Tian admitted she had known of problems with her company's products for months before informing authorities. The scandal was exposed in September.
Investigations showed that middlemen who sold milk to dairy companies were watering down raw milk, then mixing in nitrogen-rich melamine to fool quality tests for protein content.
Normally used to make plastics and fertilizer, melamine can cause kidney stones and kidney failure when ingested in large amounts. The discovery of melamine in dairy exports such as chocolate and yogurt triggered a slew of product recalls overseas.

Wednesday, January 21, 2009

MR PRESIDENT'S CARDILLAC ONE


WACHINA NUKSI, 'FEKI' MPAKA KWENYE MAYAI!

WACHINA NUKSI, 'FEKI' MPAKA KWENYE MAYAI!
During a recent raid on a wholesale centre in Guangzhou city, the capital of China 'sGuangdong province, a large quantity of fake eggs was seized. Their wholesale price is 0.15 yuan (S$0.03) each - half the price of a real egg. Consumers have a hard time telling a genuine egg from a fake one.This is good news for unscrupulous entrepreneurs, who are even conducting three-day courses in the production of artificial eggs for less than S$150. A reporter with Hong Kong-based Chinese magazine East Week enrolled in one such course. To create egg white, the instructor - a woman in her 20s - used assorted ingredients such as gelatin, an unknown powder, benzoic acid, coagulating material and even alum, which is normally used for industrial processes.For egg yolk, some lemon-yellow colouring powder is mixed to a liquid and the concoction stirred. The liquid is then poured into a round-shaped plastic mould and mixed with so-called 'magic water', which contains calcium chloride.This gives the 'yolk' a thin outer membrane, firming it up. The egg is then shaped with a mould. The shell is not forgotten. Paraffin wax and an unidentified white liquid are poured onto the fake egg, which is then left to dry.The artificial egg can be fried sunny-side up or steamed. Although bubbles appear on the white of the egg, those who have tasted it say the fake stuff tastes very much like the real thing. But experts warn of the danger of eating fake eggs. Not only do they not contain any nutrients, a Hong Kong Chinese University professor warned that long-term consumption of alum could cause dementia
MADHARA MAKUBWA ATAKAYOPATA MTU ANAYEKULA MAYAI HAYA FEKI IMEELEZWA NI KUHARIBIKA KWA MFUMO WA KUMBUKUMBU KWENYE UBONGO, YAANI MEMORY INAKUWA ZERO!!!

Tuesday, December 30, 2008

HAPPY NEW YEAR!!


May all the dreams in your eyes, all the desires in your heart and all the hopes in your life blend together, to give you the most spectacular New Year ever. Happy New Year!!!!!

Tuesday, December 23, 2008

MAHARAGE: Chakula bora kwa wenye presha, kisukari
BAADHI ya watu hawapendi kutumia maharage kama mboga kutokana na kuonekana kama ni mboga ya kimasikini, lakini kiafya maharage ni miongoni mwa mboga zenye faida kubwa mwilini na hutoa ahueni kubwa kwa watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya kama tutakavyoona leo katika makala haya;
Kwa mujibu wa utafiti mbalimbali, maharage, hasa yale meusi, ni chanzo kizuri cha kirutubisho aina ya ‘faiba’ kinachoshusha kiwango cha kolestro mwilini. Vile vile kiwango cha ‘faiba’ kilichomo kwenye maharage meusi, huweza kudhibiti kiwango cha sukari kisipande haraka baada ya chakula, hivyo kufanya maharage kuwa lishe nzuri kwa wagonjwa wa kisukari na shinikizo la juu la damu.
Iwapo utapata mchanganyiko wa maharage meusi na ule mchele ‘mweusi’ ambao haujakobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu (brown rice), basi utaweza kupata kiasi kikubwa cha protini na faiba ambacho huwezi kupata kutoka katika chakula kingine.
Aidha, utafiti wa muda mrefu uliofanywa na jarida moja lijulikanalo kama ‘Journal of Agriculture and Food Chemistry’, unaonesha kuwa mbali ya maharage kuwa na kiwango kikubwa cha ‘faiba’, pia maharage yana virubisho vingine vinavyojulikana kama ‘anthocyanins’ ambavyo hutoa kinga mwilini (antioxidant). Kiwango cha virutubisho hivyo kilichomo kwemye maharage, kinaelezwa kuwa ni kikubwa kuliko hata kinachopatikana kwenye matunda kama zabibu ambayo inaaminika kuwa na kiwango kikubwa zaidi.
Inaelezwa pia kuwa, watafiti walipofanya tathmini ya ziada kwenye maharage, waliweza kubaini kuwa maharage yanapokuwa meusi zaidi, ndivyo ambavyo kiwango kikubwa cha kinga kinavyoweza kupatikana, yakifuatiwa na maharage ya rangi nyekundu, kahawia, njano na mwisho meupe. Hii ina maana kwamba maharage meusi ndiyo yana virutubisho vingi zaidi kuliko maharage meupe na rangi nyingine.
Kwa ujumla, kiwango cha kinga (antioxidant) kilichomo kwenye maharage meusi ni mara kumi ya kile kinachopatikana kwenye matunda kama machungwa, zabibu na mengine. Hivyo unapokula maharage, siyo tu unapata ‘faiba’ ya kutosha bali pia unapata virutubisho muhimu mwilini kwa ajili ya kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya vinyelezi vya maradhi.
Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na ulaji wa maharage meusi kama ilivyothibitika katika tafiti mbalimbali za kisayansi;
MAHARAGE YANA KINGA DHIDI YA SARATANI Utafiti umefanyika na kuthibitisha kuwa maharage meusi yana uwezo wa kutoa kinga mwilini dhidi ya saratani za aina mbalimbali.
MAHARAGE KINGA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO Utafiti ulionesha pia watu wanaokula chakula chenye kiwango kingi cha ‘faiba’ kama vile maharage, hawako hatarini kupatwa na magonjwa ya moyo, ikiwemo kiharusi.
MAHARAGE HUONGEZA NGUVU MWILINI Ulaji wa maharage meusi husaidia kurejesha madini chuma mwilini na hivyo kuupatia mwili wako nguvu.
MAHARAGE YANA PROTINI NYINGI Maharage yana kiwango cha juu cha protini bora mwilini, hivyo badala ya nyama nyekundu, ambayo ikizidi ina madhara mwilini, kula maharage meusi.
Hizo ndiyo faida za maharage mwilini ambazo kila mtu anapaswa kuzijua kwa faida ya afya yake ya sasa na ya baadae.

Monday, December 22, 2008

MARRY CHRISTMASS TO YOU ALL!!



God is Love
Christmas is all about love
Christmas is thus about God and Love
Love is the key to peace among all mankind
Love is the key to peace and happiness within all creation
Love needs to be practiced - love needs to flow - love needs to make happy
Love starts with your partner, children and family and expands to all world
God bless all mankind

Saturday, December 20, 2008

VIJUE VYAKULA VINAVYOZUIA KUZEEKA
Katika toleo lake la hivi karibuni, jarida linalojishughulisha na uandishi wa habari mbalimbali za masuala ya lishe, Eating Well Magazine, limetoa matokeo ya utafiti mbalimbali wa vyakula vinavyochelewesha kasi ya mtu kuzeeka haraka, (anti aging foods) kama ifuatavyo:

CHOKOLETI Katika kisiwa kimoja cha San Blas kilichopo Panama Marekani ya Kusini, kuna jamii moja ya watu wa Kuna ambao hawana matatizo ya magonjwa ya moyo ukilinganisha na wenzao wa Panama upande wa bara ambao wanasumbuliwa na maradhi ya moyo mara tisa zaidi ya wenzao!
Sababu ya jamii moja kuwa salama kiasi hicho ni kutokana na kupenda sana kunywa kwa wingi vinywaji vitokanavyo na zao la kakao (cocoa) ambalo lina kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ‘flavanols’ ambacho kina uwezo wa kuimarisha utendaji kazi wa mishipa ya damu (blood vessels). Inaelezwa kuwa uimarishaji wa mishipa ya damu, hupunguza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo na magonjwa ya akili.

SAMAKI Miaka 30 iliyopita, watafiti wa masuala ya lishe na magonjwa, walianza kufanya utafiti wa kujua kwa nini jamii ya watu wa Inuits waliyoko Alaska walikuwa hawasumbuliwi na ugonjwa wa moyo kabisa. Katika utafiti wao, walikuja kugundua kuwa jamii hiyo inakula idadi kubwa sana ya samaki ambao wana kirutubisho cha ‘Omega-3’ kinachozuia kujijenga kwa kolestro mwilini na kuimarisha mapigo ya moyo kuwa sawa.
KARANGAUtafiti uliowahi kufanywa na madhehebu ya Wasabato, ambao husisitiza ulaji unaozingatia afya na lishe ya mboga za majani (vegetarian), unasema kuwa mtu anapokula karanga, huongeza wastani wa miaka miwili na nusu katika umri wake wa kuishi. Karanga ni chanzo kikubwa cha mafuta asili, hivyo hutoa faida sawa na zile zinopatikana kwenye Olive Oil. Pia karanga ina kiwango kikubwa cha vitamini, madini na virutubisho vingine, vikiwemo vya kukinga mwili.

MVINYO (WINE) Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kilevi kwa kiwango cha kawaida, hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, kisukari na upotevu wa kumbukumbu kichwani kutokana na umri mkubwa. Kwa mujibu wa utafiti huo, aina mbalimbali za vileo (alcohol) zinaonesha kuwa na faida hizo, lakini mkazo wa utafiti umeelekezwa zaidi kwenye mvinyo mwekundu. Inaelezwa kuwa mvinyo mwekundu una kirutubisho kiitwacho ’resveratrol’ ambacho, kwa mujibu wa utafiti, huzuia kuzeeka kwa chembechembe za mwili.

MTINDI Mwaka 1970, Georgia ya Urusi, ilidaiwa kuwa na idadi kubwa ya wazee wenye umri wa miaka 100 kuliko nchini nyingine duniani. Taarifa za wakati huo, zilidai kuwa siri ya watu wengi kuwa na umri mkubwa kama huo ni mtindi, ambao huliwa katika mlo wao wa kila siku. Wakati uwezo wa mtindi kurefusha maisha ya mtu haujathibitishwa kisayansi, lakini inaeleweka kuwa mtinmdi una kiasi kikubwa cha madini ya kashiamu na aina fulani ya ‘bacteria’ ambao hutoa kinga kwenye utumbo mdogo dhidi ya maradhi mbalimbali ya tumbo.
Mwisho, kumbuka kuwa jinsi ulivyo au utakavyokuwa baadaye, kunatokana na unavyokula, hivyo jitahidi kuwa ‘mchaguzi’ kwa kila kitu unachokula ili kulinda afya yako.

Friday, December 19, 2008

WAANDAMANA KUPINGA UUAJI WA PAKA KWA AJILI YA CHAKULA


Polisi wakiwanyang'anya raia picha zinazoonyesha paka waliokuwa-trapped kwa ajili ya kutengenezwa kitoweo.Hii ni Beijing tarehe 18 Desemba mwaka huu

Mmoja wa waandamanaji akiwa na picha ya paka waliofungiwa
Mmoja wa waandamanaji akilia kupinga matumizi ya paka kwa ajili ya chakula Beijing.


Monday, December 15, 2008

BUSH ARUSHIWA KIATU IRAQ!



Mwandishi wa habari akimrushia kiatu raisi G.W.BUSH wa marekani alipokuwa ziarani IRAQ.Jamaa alifanya ziara ya kushtukiza kwa ajili ya kuaga kabla ya kumaliza muda wake mapema january.

Saturday, December 13, 2008

MAMBO YA RUGBY!!



ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHOMWA NA MSHALE KICHWANI!!


Mwanafunzi wa umri wa miaka 11 nchini China (pichani juu), amenusurika kufa baada ya mshale uliorushwa na rafiki yake kuzama kichwani mwake kupitia kwenye jicholake, aliwahishwa hospitali huku mshale huo ukiwa bado umezama kwenyekichwa chake...kwa habari zaidi: NIFAHAMISHE.COM



Source; www.abdallahmrisho.blogspot.com






HABARI NJEMA

Kwa watu mliopo mbali na Tanzania,taarifa za habari kutoka Radio One,Radio Free Africa,Radio Uhuru na TBC zaweza kupatikana through www.dullonet.com

UMUHIMU WA NDIZI MBIVU KWENYE AFYA YAKO

Baada ya kusoma makala yangu ya leo na kuzingatia nilichokiandika, bila shaka utaanza kuingalia ndizi kwa mtizamo tofauti na uliokuwa nao hapo awali। Ndizi mbivu ni tunda maarufu sana duniani lakini ni watu wachache wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo kwenye tunda hili।Ndizi ina aina tatu za kipikee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose na Glucose na vile vile ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre) ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya muda wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda muhimu sana kwa wanamichezo. Hata hivyo, nishati siyo faida pekee unayoweza kuipata katika ndizi, ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na kuzuia matatizo mengi ya kiafya:MFAIDHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tataizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.MATATIZO WAKATI WA HEDHI (PMS)Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upunguvu wa damu kwa sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.SHINIKIZO LA DAMUTunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.NGUVU YA AKILIHivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti unaonesha kuwa potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kujisomea.KASUMBA (HANGOVERS)Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover) ni kunywa ‘Milkshake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.Mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo juu, ndizi pia husaidia katika matatizo mengine mengi kama vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa asidi tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.kHivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora, ukiilinganisha na Epo (Apple), ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili, vitamin A na chuma mara tano na vitamini na madini mengine mara mbili zaidi ya epo. Mwisho; USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU!

Sunday, December 7, 2008

EVE NDANI YA BONGO

Mwanamziki kutoka Marekani Jehan Jeffers a.k.a EVE akiongozana na mwenyeji wake Joseph Kusaga mara baada ya kuwasili TZ.Vilevile mwanamziki Fat Joe anategemewa kuwasili usiku wa leo.

EID MUBARAK WADAU!





Wadau weekend


Friday, December 5, 2008

Thursday, December 4, 2008

Mengi adai waziri ataka kumuhujumu..

TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI.

Hivi karibuni waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti alipendekeza nibambikiziwe kodi bandia ya kiasi kikubwa nitakachoshindwa kulipa na hatimaye nifilisiwe kama njia pekee ya kuninyamazisha kabisa eti kama alivyofilisiwa tajiri mmoja mkubwa huko Urusi.

Alidai kwamba vyombo vyangu vya habari vimekuwa mno mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.

Nilitegemea waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi. Angalao angefahamu kwamba anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na siyo mmiliki wa vyombo vya habari.Kama mkiristo na kama alivyoagiza Bwana Yesu namsamehe kwa vile hajui atendalo.

Baada ya kumsamehe ningetaka ajue yafuatayo.Asiyekemea maovu katika jamii, yeye ni sehemu ya maovu hayo. Waziri huyu na wale wote ambao wamekwishanitumia vitisho wakumbuke kwamba hata kama watafanikiwa kuvinyamazisha kwa hujuma zozote zile, vyombo vyangu vya habari, na hata kama mimi sitakuwepo tena, moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za wanajamii hauwezi kuzimika kamwe.

Ieleweke pia kwamba sauti za maskini na wanyonge katika jamii hazisikiki kwa urahisi. Vyombo vya habari husaidia kupaaza sauti na vilio vyao katika vita dhidi ya maovu. Ni wajibu wa kila mtu aliye na uwezo kusema kwa sauti kubwa kwa niaba ya wanyonge na maskini ili kutokomeza ufisadi.

Nachukua fursa hii kumpongeza sana Rais wetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuguswa na sauti na vilio vya wanyonge na maskini wa Tanzania kuhusu ufisadi na hatua za kijasiri zinazochukuliwa na Serikali yake dhidi ya ufisadi.

Sisi sote ni lazima tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa ujasiri, nguvu na hekima nyingi wakati huu wa majaribio makubwa.

Wednesday, December 3, 2008

JOE THOMAS, Tanto Metro & Devonte Watua




Wasanii wa Kimataifa, Joe Thomas na Danto Metro & Devonte wametua Dar jioni hii tayari kwa shoo ya muziki ya Lykizo Time Ijumaa ijayo itakayofanyika Leaders Club.