Tuesday, December 30, 2008

HAPPY NEW YEAR!!


May all the dreams in your eyes, all the desires in your heart and all the hopes in your life blend together, to give you the most spectacular New Year ever. Happy New Year!!!!!

Tuesday, December 23, 2008

MAHARAGE: Chakula bora kwa wenye presha, kisukari
BAADHI ya watu hawapendi kutumia maharage kama mboga kutokana na kuonekana kama ni mboga ya kimasikini, lakini kiafya maharage ni miongoni mwa mboga zenye faida kubwa mwilini na hutoa ahueni kubwa kwa watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya kama tutakavyoona leo katika makala haya;
Kwa mujibu wa utafiti mbalimbali, maharage, hasa yale meusi, ni chanzo kizuri cha kirutubisho aina ya ‘faiba’ kinachoshusha kiwango cha kolestro mwilini. Vile vile kiwango cha ‘faiba’ kilichomo kwenye maharage meusi, huweza kudhibiti kiwango cha sukari kisipande haraka baada ya chakula, hivyo kufanya maharage kuwa lishe nzuri kwa wagonjwa wa kisukari na shinikizo la juu la damu.
Iwapo utapata mchanganyiko wa maharage meusi na ule mchele ‘mweusi’ ambao haujakobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu (brown rice), basi utaweza kupata kiasi kikubwa cha protini na faiba ambacho huwezi kupata kutoka katika chakula kingine.
Aidha, utafiti wa muda mrefu uliofanywa na jarida moja lijulikanalo kama ‘Journal of Agriculture and Food Chemistry’, unaonesha kuwa mbali ya maharage kuwa na kiwango kikubwa cha ‘faiba’, pia maharage yana virubisho vingine vinavyojulikana kama ‘anthocyanins’ ambavyo hutoa kinga mwilini (antioxidant). Kiwango cha virutubisho hivyo kilichomo kwemye maharage, kinaelezwa kuwa ni kikubwa kuliko hata kinachopatikana kwenye matunda kama zabibu ambayo inaaminika kuwa na kiwango kikubwa zaidi.
Inaelezwa pia kuwa, watafiti walipofanya tathmini ya ziada kwenye maharage, waliweza kubaini kuwa maharage yanapokuwa meusi zaidi, ndivyo ambavyo kiwango kikubwa cha kinga kinavyoweza kupatikana, yakifuatiwa na maharage ya rangi nyekundu, kahawia, njano na mwisho meupe. Hii ina maana kwamba maharage meusi ndiyo yana virutubisho vingi zaidi kuliko maharage meupe na rangi nyingine.
Kwa ujumla, kiwango cha kinga (antioxidant) kilichomo kwenye maharage meusi ni mara kumi ya kile kinachopatikana kwenye matunda kama machungwa, zabibu na mengine. Hivyo unapokula maharage, siyo tu unapata ‘faiba’ ya kutosha bali pia unapata virutubisho muhimu mwilini kwa ajili ya kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya vinyelezi vya maradhi.
Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na ulaji wa maharage meusi kama ilivyothibitika katika tafiti mbalimbali za kisayansi;
MAHARAGE YANA KINGA DHIDI YA SARATANI Utafiti umefanyika na kuthibitisha kuwa maharage meusi yana uwezo wa kutoa kinga mwilini dhidi ya saratani za aina mbalimbali.
MAHARAGE KINGA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO Utafiti ulionesha pia watu wanaokula chakula chenye kiwango kingi cha ‘faiba’ kama vile maharage, hawako hatarini kupatwa na magonjwa ya moyo, ikiwemo kiharusi.
MAHARAGE HUONGEZA NGUVU MWILINI Ulaji wa maharage meusi husaidia kurejesha madini chuma mwilini na hivyo kuupatia mwili wako nguvu.
MAHARAGE YANA PROTINI NYINGI Maharage yana kiwango cha juu cha protini bora mwilini, hivyo badala ya nyama nyekundu, ambayo ikizidi ina madhara mwilini, kula maharage meusi.
Hizo ndiyo faida za maharage mwilini ambazo kila mtu anapaswa kuzijua kwa faida ya afya yake ya sasa na ya baadae.

Monday, December 22, 2008

MARRY CHRISTMASS TO YOU ALL!!



God is Love
Christmas is all about love
Christmas is thus about God and Love
Love is the key to peace among all mankind
Love is the key to peace and happiness within all creation
Love needs to be practiced - love needs to flow - love needs to make happy
Love starts with your partner, children and family and expands to all world
God bless all mankind

Saturday, December 20, 2008

VIJUE VYAKULA VINAVYOZUIA KUZEEKA
Katika toleo lake la hivi karibuni, jarida linalojishughulisha na uandishi wa habari mbalimbali za masuala ya lishe, Eating Well Magazine, limetoa matokeo ya utafiti mbalimbali wa vyakula vinavyochelewesha kasi ya mtu kuzeeka haraka, (anti aging foods) kama ifuatavyo:

CHOKOLETI Katika kisiwa kimoja cha San Blas kilichopo Panama Marekani ya Kusini, kuna jamii moja ya watu wa Kuna ambao hawana matatizo ya magonjwa ya moyo ukilinganisha na wenzao wa Panama upande wa bara ambao wanasumbuliwa na maradhi ya moyo mara tisa zaidi ya wenzao!
Sababu ya jamii moja kuwa salama kiasi hicho ni kutokana na kupenda sana kunywa kwa wingi vinywaji vitokanavyo na zao la kakao (cocoa) ambalo lina kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ‘flavanols’ ambacho kina uwezo wa kuimarisha utendaji kazi wa mishipa ya damu (blood vessels). Inaelezwa kuwa uimarishaji wa mishipa ya damu, hupunguza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo na magonjwa ya akili.

SAMAKI Miaka 30 iliyopita, watafiti wa masuala ya lishe na magonjwa, walianza kufanya utafiti wa kujua kwa nini jamii ya watu wa Inuits waliyoko Alaska walikuwa hawasumbuliwi na ugonjwa wa moyo kabisa. Katika utafiti wao, walikuja kugundua kuwa jamii hiyo inakula idadi kubwa sana ya samaki ambao wana kirutubisho cha ‘Omega-3’ kinachozuia kujijenga kwa kolestro mwilini na kuimarisha mapigo ya moyo kuwa sawa.
KARANGAUtafiti uliowahi kufanywa na madhehebu ya Wasabato, ambao husisitiza ulaji unaozingatia afya na lishe ya mboga za majani (vegetarian), unasema kuwa mtu anapokula karanga, huongeza wastani wa miaka miwili na nusu katika umri wake wa kuishi. Karanga ni chanzo kikubwa cha mafuta asili, hivyo hutoa faida sawa na zile zinopatikana kwenye Olive Oil. Pia karanga ina kiwango kikubwa cha vitamini, madini na virutubisho vingine, vikiwemo vya kukinga mwili.

MVINYO (WINE) Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kilevi kwa kiwango cha kawaida, hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, kisukari na upotevu wa kumbukumbu kichwani kutokana na umri mkubwa. Kwa mujibu wa utafiti huo, aina mbalimbali za vileo (alcohol) zinaonesha kuwa na faida hizo, lakini mkazo wa utafiti umeelekezwa zaidi kwenye mvinyo mwekundu. Inaelezwa kuwa mvinyo mwekundu una kirutubisho kiitwacho ’resveratrol’ ambacho, kwa mujibu wa utafiti, huzuia kuzeeka kwa chembechembe za mwili.

MTINDI Mwaka 1970, Georgia ya Urusi, ilidaiwa kuwa na idadi kubwa ya wazee wenye umri wa miaka 100 kuliko nchini nyingine duniani. Taarifa za wakati huo, zilidai kuwa siri ya watu wengi kuwa na umri mkubwa kama huo ni mtindi, ambao huliwa katika mlo wao wa kila siku. Wakati uwezo wa mtindi kurefusha maisha ya mtu haujathibitishwa kisayansi, lakini inaeleweka kuwa mtinmdi una kiasi kikubwa cha madini ya kashiamu na aina fulani ya ‘bacteria’ ambao hutoa kinga kwenye utumbo mdogo dhidi ya maradhi mbalimbali ya tumbo.
Mwisho, kumbuka kuwa jinsi ulivyo au utakavyokuwa baadaye, kunatokana na unavyokula, hivyo jitahidi kuwa ‘mchaguzi’ kwa kila kitu unachokula ili kulinda afya yako.

Friday, December 19, 2008

WAANDAMANA KUPINGA UUAJI WA PAKA KWA AJILI YA CHAKULA


Polisi wakiwanyang'anya raia picha zinazoonyesha paka waliokuwa-trapped kwa ajili ya kutengenezwa kitoweo.Hii ni Beijing tarehe 18 Desemba mwaka huu

Mmoja wa waandamanaji akiwa na picha ya paka waliofungiwa
Mmoja wa waandamanaji akilia kupinga matumizi ya paka kwa ajili ya chakula Beijing.


Monday, December 15, 2008

BUSH ARUSHIWA KIATU IRAQ!



Mwandishi wa habari akimrushia kiatu raisi G.W.BUSH wa marekani alipokuwa ziarani IRAQ.Jamaa alifanya ziara ya kushtukiza kwa ajili ya kuaga kabla ya kumaliza muda wake mapema january.

Saturday, December 13, 2008

MAMBO YA RUGBY!!



ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHOMWA NA MSHALE KICHWANI!!


Mwanafunzi wa umri wa miaka 11 nchini China (pichani juu), amenusurika kufa baada ya mshale uliorushwa na rafiki yake kuzama kichwani mwake kupitia kwenye jicholake, aliwahishwa hospitali huku mshale huo ukiwa bado umezama kwenyekichwa chake...kwa habari zaidi: NIFAHAMISHE.COM



Source; www.abdallahmrisho.blogspot.com